Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010

PICHA NA MICHUZI JR-SAME MASHARIKI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...