Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa  uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto  maeneo ya milimani kilomita  kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wakiambiwa waende wakajifunze udereva wanazira haya ndio matokeo yake, tz ndio inaongoza kwa ajari za magari duniani

    ReplyDelete
  2. Duh jaman hali inatisha Mungu atusaidie

    ReplyDelete
  3. Hawa watu watatumaliza kweli, dah mbona mtihani! kla cku basi ajali hizo au hayo magari huendeshwa na nguvu za kiza?

    ReplyDelete
  4. Ni kweli mdau wa kwanza. Kwani ni juzi tu walifurahia maandamano yao kupatiwa ufumbuzi wakijua wameshinda, leo janga hili sasa sijui tuseme nini, serikali inajitahidi kutafuta mbinu fulani kulinda wasafiri, madereva wanaona kama serikali inawaonea. Haya sasa tuone hili na ajali zitaendelea tu kwani madereva wanasifa sana wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. Na wengine hawana elimu kabisa ya umakini wawapo barabarani

    ReplyDelete
  5. ANONYMOUS, nani kaKUdanganya kusoma ndio kutatua matatizo ya ajali, je amuangalii miundo mbinu mibovu ya mabarabara,kuwa ni chanzo pia cha ajali Au katika kubadilisha leseni za awali madereva wengi walisoma lakini bado ajali ziliendelea kutokea? tambua kusoma kwa madereva ni mradi unaoanzishwa na mtu ili ajipatie kipato na ajali inapotokea lawama uhenda kwa dereva kwa nini baadhi ya lawama zisiende kwa selikali kwa kujenga barabara mbovu na vyombo vya usafiri vikiwa havina ubora. anonymous badilika usifate mkumbo na kukalili kila mzungu ni padri.

    ReplyDelete
  6. hakuna elimu ya practical Tanzania....hakika hata wakienda kusoma wakirudi na A'S Za kila cozi haitopunguza ajali...by the way dereva bora ni yule mwenye experience na sio mabanda..(A)...Mi nadhani likitokea tatizo liwe linatupa somo kuhusiana na ubora wa barabara zetu..moja,ninaimani kwamba mashimo yaliyosabaisha ajali ya majinja express pale mafinga,yameshafukiwa na mashimo mengine yote ya barabarani tz yafukiwe....pili..

    ReplyDelete
  7. kweli inatisha,jamani hembu tazameni picha ya pili kutoka mwisho kwa umakini kuna vitu vya ajabu vinaonekana katika picha hiyo ambayo havielewike na vinatisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...