Baadhi ya waandishi walioudhuria uzinduzi wa simu mpya ya Huawei Ascend P8, iliyozinduliwa hivi karibuni jijini London 

KAMPUNI nguli sekta ya teknolojia  ya habari na mawasiliano ya Huawei imezindua simu mpya aina ya Ascend P8 ikiwa ni muendelezo wa kampuni hiyo kuleta mapinduzi kwenye nyanja ya mawasiliano ulimwenguni.
 
Akizungumza kwenye uzinduzi wa simu hiyo kimataifa uliofanyika kwenye jiji la London, Uingereza mwishoni mwa wiki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Bw. Richard Yu alisema uundwaji wa simu hiyo ulilenga kurahisisha zaidi mahitaji ya teknolojia ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu hizo.
 
“Na hiyo ndiyo sababu kila mfumo wa simu hii upo kisasa zaidi kuanzia muonekano wake ambao kiukweli ni ‘bapa’ kwa milimita 6.4 ili kurahisisha ushikwaji wake, rangi zake zenye mvuto sambamba na  kamera yenye uwezo wa hali ya juu yenye kukidhi kiu ya kiubunifu kwa kila mtumiaji wake,’’ alifafanua.
 
Kwa mujibu wa Bw. Yu simu hiyo ambayo inaingia sokoni ikiwa na rangi tofauti nne za dhahabu, nyeusi, fedha na kijivu imeboreshwa zaidi ikiwemo kwenye mfumo wake wa ‘kutafutwa kwa sauti’.
 
“Ni rahisi zaidi kwa mtumiaji wa simu hii kuiita kwa sauti na kugundua sehemu ilipo hususani pale inapotokea kwamba amesahau alipoiweka au katika mazingira yoyote yakiwemo yale yanayohusisha wizi kwa wakati husika,’’ alisema.
 
Akizungumzia ubora wa betri ya simu hiyo Bw. Yu alisema umezingatia matumizi ya muda mrefu ambapo kwa mtumiaji ‘king’ang’anizi’  anaweza kutumia kwa siku nzima bila kuichaji huku kwa wale watumiaji wa kawaida anaweza kuitumia kwa siku moja na nusu.

“Mapinduzi mengine kwenye simu hii yanajidhihirisha kwenye mfumo wake wa ‘kioo mguso’  yaani ‘screen touch’  ambao umeboreshwa zaidi huku pia mfumo wa kamera ukiboreshwa hususani katika uchukuaji wa picha za ‘selfie’ ambapo imehusisha aina tatu tofauti za picha za aina hiyo,’’ alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...