Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia  kutokana na kukamilika  kwa miundombinu  ya mitambo ya  umeme ifikapo machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika ziara ya  ukaguzi wa miradi ya umeme ya  Kurasini, Mbagala pamoja na Kinyerezi  jijini Dar es Salaam leo.

Ziara hiyo  iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la  kusogeza miundombinu ya umeme karibu na watumiaji wa umeme.

Simbachawene amesema kuwa  kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa uhakika  inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n amatatizo ya  umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  amesema kuwa matatizo mbalimbali ya  ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa  kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  kuhusiana na uboreshaji wa  Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2015

    Liwe historia na maafisa usiku wapange na kuwekeza tukijua kuwa baada ya muda idadi ya watu inaongezeka na wanahitaji huduma, bila kuwekeza tukitarajia maendeleo na ongezeko la watu tatizo litajirudia miaka ijayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...