Habari zilizotujia hivi punde zinasema Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku itayotajwa kesho na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.

Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.
Mjane wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, Ngeme Mbita (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo.  Brigedia Mbita amefariki leo katika Hospitali ya Lugalo. (Picha na Francis Dande).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Roho yake ipumzike katika Amani ya Milele mikononi mwa Mwenyezi Mungu, Amina.

    ReplyDelete
  2. May his soul rest in eternal peace! General Mbita was a true son of Africa.

    ReplyDelete
  3. Innaa lillaahi wainnaa ilayhi raajiun.Allah amsamehe makosa yake na amuingize peponi.ajaalie azikwe kesho,asiekwe sana kama inavyoanza kuzoeleka.amin

    ReplyDelete
  4. May he rest in peace. It's a pity that he has gone while witnessing the current Xenophobia in South Africa as a "Thank You Note" For His Sweat in the South Liberation Struggle. I know that Mugabe is in mourning.

    ReplyDelete
  5. May your soul rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  6. Mungu ampumizishe mahali pema. Ila ukombozi wake ulikuwa hauna maana manake tunaona sasa Afrika ya Kusini inavyowabagua afrika wenzio.

    ReplyDelete
  7. Inna Lillah Waynna Illahy Rajioun.

    ReplyDelete
  8. Inna Lillah.......
    Mungu amfungulie pepo kwa kazi alizofanya na misaada aliyowapa binAdam wenzake hapa duniani.He was an achiever and I remember him from Tabora Boys
    God give peace of mind to his family and friends.
    Ibrahim Manthy.

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wafiwa Mungu awatie nguvu wakati huu wa msiba. Huyu mzee wa changombe uhindini/TCC tumekaa naye vizuri yeye na jamii yake siku nyingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...