Na Bashir Yakub.
Ukisoma kichwa cha habari utaona nimeongelea nyumba lakini kimsingi mchakato huu unahusisha mali zote za wanandoa vikiwemo viwanja, magari, na kila kitu ambacho ni mali ya wanandoa. Kichwa kinajieleza kuwa ni makosa benki au taasisi yoyote ya fedha kuuza nyumba au mali yoyote ya wanandoa ikiwa wakati wa kuchukua mkopo mwanandoa mmojawapo hakushirikishwa katika mchakato wa mkopo huo.
1. MAANA YA MALI YA WANANDOA.
Mali ya wanandoa ni mali yoyote ambayo imepatikana kwa nguvu au juhudi za pamoja kati ya mme na mke walio kwenye ndoa ya kikristo, kiislam, ya serikali au ndoa nyingine yoyote halali ikiwemo ile ya kuishi wote kwa muda wa miaka miwili ( presumed marriage ). Hizi zote ni ndoa ambazo mali ikipatikana ndani yake huwa ya wanandoa. Pia ile mali ambayo mmoja wa wanandoa amekuwa nayo kabla ya ndoa lakini baada ya ndoa ikaendelezwa na wanandoa kwa kiasi kidogo au kikubwa nayo hubadilika kuwa ya wanandoa wote.
Hii inajumuisha mali zilizopatikana kabla ya ndoa lakini wanandoa wenyewe wakaamua kwa hiari yao kuzifanya kuwa zao wote kwa pamoja kama familia kwa makubaliano maalum. Nalazimika kutoa ufafanuzi huu ili ninaposema mali ya wanandoa hairuhusiwi kuuzwa ieleweka hata kwa kiwango kidogo mali zipi ni za wanandoa na hivyo kuhitaji ridhaa ya wote katika kuwekwa dhamana.
2. MIVUTANO KATI YA TAASISI ZA MIKOPO NA WANANCHI.
Kipindi cha hivi karibuni hasa baada ya kuongezeka wito wa ujasiriamali mali na wingi wa taasisi za fedha kumekuwepo na kesi nyingi sana kati ya raia na taasisi hizi za fedha. Unapoangalia kesi hizi kwa haraka unaweza kugundua mambo mawili, kwanza umakini mdogo wa taasisi za fedha hasa katika ufuatialiaji wa uhalali wa dhamana na pili uelewa mdogo wa raia kuhusu taratibu na haki walizonazo katika mikopo. Raia wanazilalamikia taasisi za mikopo kwa kuwa wababe , wasio na subira na wakiuka taratibu na huku taasisi za fedha nazo zinawalaumu raia kwa kuwa wakaidi ,wakorofi na wasiopenda kurejesha amana wanazopewa. Ni msuguano mtupu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...