Na Bashir Yakub.
Kuna malalamiko katika baadhi ya maeneo na zaidi malalamiko haya yamekuwa yakielekezwa kwa mamlaka za serikali za mitaa. Nimewahi kuandika kuhusu ukiukaji wa taratibu mbalimbali ambao hufanywa na serikali za mitaa katika maeneo au ardhi za watu. Pia niliandika kuhusu upotoshi wa mamlaka za serikali za mitaa katika kuwaandalia watu mikataba ya mauzo ya ardhi wakati wakijua kuwa hawaruhusiwi kufanya hivyo jambo ambalo huwasababishia wananchi usumbufu mkubwa wanapoamua kutafuta hati au kubadili majina kwakuwa mikataba hiyo ya serikali za mitaa huwa haikubaliki kisheria na hivyo watu hurudishwa kuibadili.
Leo tena nazungumzia ubabe walionao serikali za mitaa wa kutwaa maeneo ya watu na kuyapangia shughuli mbalimbali za mtaa huku yakiwa ni maeneo ya watu binafsi. Kugeuza maeneo ya watu njia bila fidia ni moja ya uonevu mkubwa ambao wamekuwa wakiupata wananchi kutoka serikali za mitaa. Kwa ufupi tutaangazia jambo hilo likoje kisheria.
1.SERIKALI ZA MITAA HAWARUHUSIWI KUTANGAZA ENEO FULANI KUWA NI NJIA.
Serikali za mitaa hawana mamlaka kisheria kuchukua eneo la mtu kulitangaza kuwa njia. Kinyume na ilivyozoeleka ambapo viongozi wa serikali za mitaa hutembea maeneo mbalimbali ya mtaa na kuchukua maeneo ya wananchi kwa madai kuwa yanapaswa kuwa njia. Sheria ya ardhi inasema kwamba serikali kuu au serikali ya mtaa au chombo chochote hakiruhusiwi kutenga maeneo kuwa njia isipokuwa lazima watume maombi kwa kamishna wa ardhi ambaye ndiye atakuwa na mamlaka ya kutangaza eneo fulani kuwa ni njia.
Sheria inaendelea kusema kuwa maombi hayo yatakuwa yamewekwa katika fomu maalum na kujazwa katika namna inayokubalika. Kwa hiyo kumbe hali haiko kama tulivyozoea ambapo serikali za mitaa huamua kuchukua eneo la mtu na kulifanya njia bila ruhusa ya kamishna wa ardhi. Ieleweke kuwa utaratibu ndio huo wa kutuma maombi kwa kamishna wa ardhi na si kuamka asubuhi na kulifanya eneo la mtu kuwa ni njia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...