Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Philip Mangulla akizungumza na wanafunzi na waalimu wa shule ya Hagafilo mkoani Njombe kuhusiana na katiba pendekezwa na utofauti kati ya katiba pendekezwa na ya sasa.
wanafunzi na waalimu wakimsikiliza Makamu mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula juzi wakati akiwapa ufafanuzi wa katiba Pendekezwa.(picha na furaha eliabu wa www.eliabu.blogspot.com)

Na Furaha Eliab, Njombe

MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) - Bara, Philip Mangula amesema kuwa viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba pendekezwa na kuwataka wamuonyeshe kipengele kinacho taja masuala ya dini na mahakama ya Kadhi.

Akizunzungumza na wanafunzi wa sekondari, Chuo na walimu katika shule ya Hagafilo Mkoani Njombe wakati akitoe elimu ya katiba pendekezwa , amesema kuwa ameisoma katika yote na hajaona kipengele kinacho zungumzia masuala ya udini wala mahakama ya kadhi.

Lakini hata hivyo viongozi wa dini wanapinga mswada wa mahakama ya kadhi kupitishwa bungeni na kuwa sheria.

Amesema kuwa alikuwa katika kanisa moja anako Sali mchungaji wake alisema kuwa waumini wasiipegie kura katiba pendekezwa kwa kuwa ina masuala ya Mahakama ya Kadhi alipo muuliza ni katika kipengele gani kinacho zungumzia mahakama hiyo mchungaji huyo hata kipengele hicho alisema hakifahamu.

 Amesema kuwa katiba hiyo haina kipengele hata kimoja kinachozungumzia dini yoyote na kunakipengele kinacho zungumzia utawala wa sheria na kuwapo kwa mahakama huru

Amesema kuwa katika katiba pendekezwa kuna misingi ya utawala bora na umiliki wa arhi na kuwa ardhi hiyo inatunza na kuwa ni mali ya mtanzania wa kizazi cha sasa na cha baadae.

Katika hatua nyingine Mangula ameungana na kauli ya kiongozi katoriki Kadrinari Polinal Pengo kuhusiana na kuwahusu wananchi kuchukua maamuzi yao wenyewe juu ya kupiga kura ya ndio au hapana.

Amesema kuwa wananchi wakiisoma katiba wao wenyewe wakaielewa kama kuna mapungufu watayaona waikatae wao wenyewe na wanao sema isipigiwe kura wawe na hoja kwanini isipigiwe kura na sio wanasema hivyo bila kuwa na hoja sahihi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...