Kamishna wa Forodha na Ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Masamaki Kabisi akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo bandarini(TANCIS) ikiwa unasaidia katika kufanya makadirio ya kodi sahihi kulingana na taarifa sahihi zilizoletwa kwa kutumia mfumo huo, pia utasaidia wateja kujua sehemu mizigo yao ilipo na pia wanapaswa kulipa kiasi gani kulingana na mzigo wa mteja, wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Felix Tinkasimile akiwaeleza waandishi wa habari namna mfumo mpya wa uondoshaji mizingo unavyoongeza uwazi na uwajibikaji utakaosaidia kuzuia upoteaji wa mizigo bandarini ikiwemo Magari na Makontena , wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari majukumu ya kituo hicho ikiwemo kutoa tathnimi ya kodi unayopaswa kulipwa kwa kupitia na kuhakiki nyaraka zote kutoka kwenye kadhia zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kutozwa.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy wakati wa Ziara iliyofanyika katika mamlaka hiyo kuona jinsi mfumo wa TANCIS unavyofanya kazi.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...