Mkazi wa Kawe jijijini Dar es Salaam Irene Mrema ameibuka kuwa mshindi wa kitita cha fedha taslimu shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. 
Mrema ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) amesema kuwa amefurahia ushindi huu na ana imani kitita alichojishindia kwa kiasi kikubwa kitayabadilisha maisha yake kuwa bora zaidi.”Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni kwa ushindi huu nimeamini kuwa Jaymillions sio promosheni ya mzaha na matangazo bali ya ukweli na nawasihi watanzania wenzangu tuchangamkie fursa hii”.Alisema kwa furaha. 
 Promosheni ya Jaymillions inayoendelea ikiwa inakaribia kufikia mwisho imeishawawezesha baadhi ya wateja wa Vodacom kuwa mamilionea kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi watatu wa milioni 100/-washindi watano wa milioni 10/-na washindi 40 wa milioni 1/-na maelfu ya wateja wameishajishindia muda wa maongezi. 
Washindi wa milioni 100/-ni Uwezo Madegenge kutoka wilayani Kilolo mkoani Iringa , Khamis Khalid na mshindi wa leo Irene Mrema. Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, amewahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymiilions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda. 
 Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/- 
 “Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda hasa kipindi hiki ambacho promosheni inaelekea ukingoni.” alisema Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati alipokuwa akimtangaza mshindi wa shilingi milioni 100  mwishoni mwa wiki kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Irene Mrema mkazi wa Kawe jijini Dar es Salam(30) alijishindia kitita hicho.Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini Jehud Ngolo.Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...