Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, anayefuata ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania. Rodriguez alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...