Benki ya NMB imefungua rasmi tawi lake jipya la Singida. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote. Tawi hili limefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk. Perseko Vincent Kone.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida- Mh. Dk. Perseko Vincent Kone (kati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la Singida, kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati Bw. Ole Loibanguti na Meneja wa NMB tawi la Singida- Bi. Christine Mwangoma.

Kufunguliwa kwa tawi la Singida sasa kutaharakisha maendeleo ya wakazi wa Mkoa wa Singida na pia kurahisisha biashara kati ya wananchi wa mji huo na wa maeneo ya jirani. 

Hii ni kwa sababu   NMB sasa inawezesha wateja wake kuuza, kununua, kutuma na kupokea fedha za kigeni popote ulimwenguni tena kwa gharama nafuu. Kwa hili biashara itaimarika na ubadilishaji wa fedha za kigeni utakuwa rahisi kupita hapo awali, hasa tukifahamu kua Singida ni sehemu ya biashara na wafanyabiashara mbali mbali hutembelea mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida- Mh. Dk. Perseko Vincent Kone  akipata maelezo kuhusu huduma  na bidhaa zinano tolewa katika tawi hilo kutoka kwa Meneja wa NMB tawi la Singida - Bi. Christine Mwangoma.

Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB imetoa shilingi Milioni 25 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Singida kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.

NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 160, ATM zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na idadi kubwa ya wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...