Mkurugenzi wa Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,Salim Abdullah akisaini makubaliano ya kuendeleza utafiti  tasisi hiyo kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Kinga na wa China,Dk.Ning Xiao  katika hafla iliypfanyika leo jijin Dar es Salaam.(Picha Emmanuel Massaka).
 WAZIRI wa Afya  na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid akizungumza hafla ya makubaliano na Serikali ya watu wa China ( Kulia),Naibu Waziri  na Kamisheni ya Taifa ya Afya na Uzazi wa Mpango,na  Usimamizi wa Tiba Asili iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakishuhudia kutiliana saini kati ya Serikali na China katika suala zima la kuwekeza katika utafiti wa Tiba asili.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Serikali imesema itaendeleza kufanya utafiti wa tiba asili ikiwa ni pamoja na kuanzisha baraza la tiba asili ,kutokana na kuwepo kwa mafanikio ya kutumia dawa hizo.

Hayo aliyasema leo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid wakati akisaini makubaliano na Kamisheni ya Taifa ya Afya na Uzazi wa Mpango na  Usimamizi wa Tiba Asili ya China,katika kuendeleza Wizara ya Afya  katika nyanja ya utafiti,ujenzi  wa kituo cha Moyo.

Amesema makubaliano hayo  yataongeza  chachu kwa Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii, katika maeneo ambayo kwa sasa Wizara imeongeza mkazo katika utafiti,hivyo kutokana na makubaliano   yaliyofanyika kutaongeza kasi.

Dk.Seif amesema kuwa madaktari kutoka nchini china wamekuwa wakija katika kutoa huduma nchini hali ambayo inaonyesha ushirikiano katika sekta ya afya katika kuhudumia wananchi.

Amesema katika matumizi ya dawa za asili nchi ya China iko mbali ambapo wameweza kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hata mnapowekeza huko msikubali wenye kutangaza matibabu mbadala kutangazao matangazo yanayosema dawa za hospitali ni sumu kwa sababu siyo kweli na hii inaweza kupotosha jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...