Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya
tarehe 10, Aprili mwaka huu, itashuka
dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).
Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia
kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na
mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika
mwaka huu.
Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini
Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa
na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
Mshindi wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa
fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya nchini Congo - Brazzavile kuanzia
Septemba 13 mwaka huu.
VPL KUENDELEA JUMAMOSI
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa
wiki katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na michezo
mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar
watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal
Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya
Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la
Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa
Mabatin uliopo Mlandizi.
Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka
Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa
wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro
kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
KILA LA KHERI YANGA.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi
amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la
Shirikisho barani Afrika (CC) Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi
ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo
Gweru Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi
walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka
ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia
katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de
Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...