Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi
Christopher Chiza, akitoa hotuba yake baada ya ufunguzi wa kongamano la Biashara na
Uwekezaji kati ya nchi ya Comoro na Tanzania kwa wadau na wafanyabiashara kutoka
Tanzania (hawapo pichani). Kongamano hilo limeanza tarehe 23 Aprili, 2015 likiwa na
lengo la kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na Comoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi
Christopher Chiza (mwenye suti ya bluu) Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.
Ikililou Dhoinine (mwenye mavazi meupe) pamoja na viongozi, wafanyabiashara na
wadau kutoka Sekta Binafsi baada ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji
kati ya nchi ya Comoro na Tanzania lilioanza tarehe 23 Aprili, 2015.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi
Christopher Chiza (Mb) amewaeleza wananchi wa Visiwa vya Comoro pamoja na
wafanyabiashara kuwa Serikali ya Tanzania imejithatiti katika kuboresha wigo mpana
katika masuala ya ili kuweza kukuza uchumi na uwekezaji nchini.
Amesema hayo akiwa anatoa Hotuba yake kwa Wadau na Wafanyabiashara kutoka
Tanzania baada ya ufunguzi wa Komango la Biashara kati ya Comoro na Tanzania jana
Alhamisi tarehe 23 Aprili, 2015.
“Miongoni mwa maeneo ambayo Serikali ya Tanzania imeweza kuyaboresha ili
kurahisisha na kuongeza uwekezaji ni pamoja kujenga Miundombinu bora yaani
Barabara, kuboresha Viwanja vya Ndege, Bandari itarahishisha uchukuzi na kuongeza
fursa katika nchi SADC”, alisema Waziri Chiza.
Chiza aliongeza kuwa, mazingira ya kibishara kwa Tanzania yanalindwa na Sera zilizopo
kwa kupitia Sera ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi yaani (PPP) inalinda na
kusimamia masuala ya uwekezaji baina Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Wafanyabiashara kutoka nchini Tanzania wametaja baadhi ya changamoto
zinazowakabili ikiwa ni pamoja na pamoja na ushuru wa forodha kuwa mkubwa visiwani
Comoro, Usafiri usio wa uhakika unaosababisha bidhaa zao kuharibika mara kwa mara
pamoja na mahitaji ya viza kuingia na kutoka nchi Comoro.
Mapema wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Rais wa Visiwa vya Comoro Ikililou
Dhoinine amesema, “tayari ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yake ishirikiane
na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania kwa lengo la kuondoa matumizi ya viza baina
ya Tanzania na Comoro ili kuweza kurahisha masuala ya biashara katika nchi hizi.
Waziri Chiza alimalizia kwa kusema kuwa, Visiwa vya Comoro vina fursa nyingi za
uwekezaji na biashara ikiwemo huduma ya usafiri wa majini, anga pwani zenye madhari
kwa uwekezaji wa Hoteli za kimataifa, ambapo amewashauri wawekezaji wa Tanzania
kutumia fursa ya mkutano huo kuyabaini na kuyafanyia kazi.
Imetolewa na Francisca Swai
Afisa Habari
Ofisi ya Waziri Mkuu,
24 Aprili,2015
Boresheni miundombinu ya barabara. Barabara ni nyembamba sana Tanzania kiasi cha kusababisha ajali kila kukicha. Na hili Tanzania inaweza kabisa bila kulipinga. Barabara ndo chanzo kikuu cha ajali za barabarani
ReplyDelete