Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia vifo vya mashabiki wa klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani eneo la Makunganya mkoani Morogoro.
Katika salamu zake Rais Malinzi amesema, TFF imezipokea kwa masikitiko taarifa hizo za ajali na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wanawapa pole wafiwa wote na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze kupata nafuu na kupona kwa uharaka zaidi.
Aidha Rais Malinzi ameagiza michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itakayochezwa wikiendi hii nchini, kusimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...