Na Avila
Kakingo, Globu ya Jamii.
WANANCHI watatu kati ya kumi wameshakumbana na wizi ndani ya kipindi cha mwaka jana,na asilimia 84 ya wananchi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuathiriwa na
makundi ya vijana waharifu kama panya road.
Hayo yameelezwa kwenye Utafiti umefanywa na Twaweza kwenye utafiti wenye jina la Je, tuko salama? maoni ya wananchi juu ya usalama na haki waliofanya mkutano katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Mtafiti wa
twaweza Elvis Mushi amesema kuwa licha ya kuongezeka kwa matukio ya vurugu za
kisiasa pamoja,wizi na hofu juu ya makundi ya vijana ya wahalifu wananchi wengi
wamekuwa hawana usalama wao katika maisha wanayoishi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidani Eyakuze aliongezea kuwa kwanza wananchi wengi wanahisi kuwa salama
maeneo yao lakini bado wanakumbana na vitendo vya wizi, wanaogopa kuvamiwa na panya road na baadhi yao kushuhudia ghasia na vurugu za kisiasa.
Aidha watu wameshuhudia ongezeko la ukatili dhidi vya vituo vya polisi ndani ya miaka miwili iliyopata, jambo hili linapunguza imani yao na vyombo vya usalama.
Aidha watu wameshuhudia ongezeko la ukatili dhidi vya vituo vya polisi ndani ya miaka miwili iliyopata, jambo hili linapunguza imani yao na vyombo vya usalama.
Eyakuze aliongeza kuwa usalama una umhimu wa
kipekee katika masuala ya kijamii na kiuchumi akiwa na akiwa na rai kwa
serikali kuyazungatia maoni haya ya
wananchi katika utekelezaji wa jukumu lake la kuwahakikishia wananchi usalama
wa hali na mali.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu) (CAG), Ludovick Uttoh
akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari katika viwanja vya
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii).
Ofisa
masoko wa Twaweza Costantine Magavilla akizungumza leo na wajumbe
kutoka makampuni mbalimbali katika mkutano wa Twaweza uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam,(kulia)
ni Mtafiti wa Twaweza Elvis Mushi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze akiuliza swali kwa wajumbe
waliohudhuria katika mkutano wa Twaweza leo katika ukumbi wa mikutano wa
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam kushoto ni Mkurugezi wa
Capacitate Consulting, Ngasuma Kanyeka.
Baadhi
ya wajumbe kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Twaweza
katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam
leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...