JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
 TAARIFA KWA UMMA
YAH: UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO
WA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
_______________

Kesho Jumatano tarehe 29 Aprili, 2015 Wabunge wote kwa ujumla wao watakutana katika Ukumbi wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam kupokea Mapendekezo ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 kwa mujibu ya matakwa ya Kanuni ya 97 ya kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013.

Shughuli hiyo itaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi kwa Waheshimiwa Wabunge na Washiriki wote kuwasili na kuketi Ukumbini kabla ya ukaribisho utakaotolewa na Naibu Spika amabaye pia atakuwa mwenyekiti wa Mkutano huo na kufuatiwa na neno la utangulizi kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Aidha, Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yatafanyika kuanzia saa nne asubuhi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahususiano na Uratibu) Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb) na kufuatiwa na uwasilishwaji wa mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (Mb).

Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa sita mchana, na baadae kamati za Bunge kuendelea na utekelezaji Majukumu yake kulingana na ratiba za kamati.


Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
28 Aprili 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...