Na Ripota Maalum.

Serikali ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasaidia vijana wa Tanzania katika kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira kwa kuwapa maarifa na mikakati ya kujiajiri na kujinadi kwa waajiri .

Vikwazo vinavyowakabili vijana katika soko la ajira ni pamoja na kutokuwa na maarifa ya kupata kazi na tabia ambazo zitawawezesha kuwa karibu na wafanyakazi wenzao,kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo kuweka heshima na mwisho kuwa wawakilishi bora wa taasisi wanayotumikia .

Kwa kutambua changamoto hizo Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka taasisi ya Restless Development Organization (ICS)kuwafundisha vijana mikakati ya kujinasua na matatizo hayo .

Wakizungumza katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) walimu hao wa kujitolea wamesema wanawafundisha vijana namna ya kuandika wasifu wao wenye maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu, ujuzi na kujiajiri wenyewe .
Kiongozi wa walimu (ICS) Gemma Bunn aliliambia gazeti hili kwamba sababu ya kuwapo hapa nchini ni kwa kutambua kuwa Tanzania ina vijana zaidi ya asilimia 50 ambao hawawezi kupata ajira na wengi hukwama kutokana na vigezo kama hivyo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya yaani mtu anakuja kuwafundisha watu kuandika Cv kisha anapewa media....yaani tabu tupu, ukawa wanaelimisha watu umuhimu wa kujiandikisha daftari la kudumu hata taarifa zao hazipatikani, kama nia ni kupunguza ukosefu wa ajira bwana shigongo pilika zake tunaziona za kuwaelimisha watanzania, halikadhalika mzee mengi, lazima tuwe makini si kila kinachofanywa na watu toka nje kina mshiko, hili lingefanywa na mwananchi lisinge andikwa.......

    ReplyDelete
  2. Ndo shida za ma-graduate wa shule na vyuo vya kata. Ukichelewa kumkunja samaki akiwa mbichi ndo basi tena!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...