th5Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
th2Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.th3Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.th4Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2015

    Takwimu tulizonazo zitumike na ngazi zote za serikali kama kigezo cha kupanga maendeleo na kushughulikia mahitaji na huduma muhimu za kuboresha maisha ya wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...