kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Hali ya Sintofahamu imeukumba mji wa Tengeru leo Asubuhi baada ya wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi Kufunga barabara kwa muda wa masaa mawili na kuacha shughuli za maendeleo kusimama kwa muda huku magari  ya abiria yanayokwenda katika mikoa ya Kilimanjaro,Tanga na Dar es salaam na mji mdogo wa usa river na maeneo mengine kupata adha hiyo.

Wanafunzi hao walizuia bara bara hiyo  wakishinikiza madai yao kusikiliza kwani wameshatoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo hicho bila ya kushughulikiwa kwa muda sasa wakiainisha kuwa wamekuwa wakipatiwa adhabu zisizo stahiki ikiwemo kurushwa kichura kuchapwa makofi huku kanuni za utumishi zikivunjwa na uongozi wa chuo hicho cha ualimu Patandi kilichopo wilayani Meru..

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti na libeneke la kaskazini  blog  Mmoja wa wanafunzi  Jenny Mlay  alisema kuwa leo Asubuhi mkuu wa chuo alimkuta mwanafunzi mwenzao amelala bwenini akiumwa na kuacha taa ikiwa inawaka na ndipo alimpiga makofi na wao kwa umoja wao wakaamua kuingia barabarani ilikufikisha kilio chao cha muda mrefu.

Alisema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji wa wanafunzi kwa kupewa adhabu zisizoendana na maadili ya vyuo ikiwemo kupiga magoti,kuruka kichura, na nyingine kama hizo ambazo ni kinyume na haki za binadamu na kanuni za chuo.

“Utakuta mtu anarukishwa kichura tena muajiriwa ambaye amekuja kuongeza daraja hapa chuoni huyu sio mwanafunzi wa darasa la kwanza hivyo tumefikisha ujumbe wetu mara nyingi kwa uongozi lakini hatupatiwi majibu ndio tukaamua kufunga barabara ilikufikisha ujumbe wetu kuwafikia walengwa”alisema Mlay
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hawa wajinga sana sasa barabara inahusiana na nini na hizo adhabu zao chuoni..wao walitakiwa ku deal na chuo na walimu wao sio kuwaumiza wasafiri wasio na hatia...

    ReplyDelete
  2. Yaani bado ukoloni wa kuchapwa viboko na kurushwa vichura upo mpaka leo? tena kwa wanafunzi wa vyuo jamani Tanzania. Rekebisheni hili jamani heshima ni kitu cha msingi sana. Mkuu wa chuo hata aibu unamchapa makofi mwanafunzi tena wa chuo? shame on you baba or mama. Lol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...