Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Baraza la Biashara la China na Afrika (CABC) Tawi la Tanzania,Xian Ding akizungumza na waandishi wa habari  katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau katika katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye amesema kukutana na watu wa China ni fursa  nzuri ya watanzania katika kushirikiana katika sekta ya uwekezaji nchini.

Simbeye amesema hayo katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Simbeye amesema wachina hawaji Tanzania kutembea bali wanakuja kwa ajili ya kukuza viwanda vyao vilivyopo nchini ,hivyo ni fursa kwa wawekezaji watanzania kuweza kukutana na wachina hao ili kushirikiana nao.
  
Naye Mwenyekiti wa  Baraza la Biashara la China na Afrika (CABC) Tawi la Tanzania,Xian Ding amewataka wachina pamoja na watanzania kuzidisha ushirikiano ili kupata maendeleo katika biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...