Kundi la Watanzania 25 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunaipongeza sana serikali ya Tanzania kuwajali watanzania pindi wawapo nje ya nchi na wakati machafuko yatokeapo. Tunaomba iboreshe ajira za wananchi ili watu wengi na hasa vijana wapate ajira, wajiajili wenyewe na kutulia nyumbani.

    ReplyDelete
  2. Big up Mhe Membe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...