Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akionyesha tuzo yake mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),aliyotunukiwa kwa mchango wake mkubwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii,katika tamasha la pasaka.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika tamasha la 15 la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutubi maelfu ya watu waliohudhuria Tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.
Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.
Mwanamuziki
wa Kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca
Malope akicheza na shabiki wake kwa staili ya pekee kabisa,huku uwanja
ukilipukwa na mayowe kila kona.
Mwimbaji nguli wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu pichani kulia akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja katika lamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Kwaya
ya Kijitonyama wakiimba katika tamasha la 15 la Pasaka,
lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015.
Sehemu ya umati wa Watu waliohudhuria tamasha la 15 la
Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
Jumapili 5, 2015.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe wakimkaribisha jukwaani Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe pichani kulia ni Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...