Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwasili hotelini nchini Kuwait kwa ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait na Mkurugenzi Mkuu wa Kuwait Fund.Anayeongozana na Waziri Membe (mwenye kanzu nyeupe) ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib ambaye alimpokea uwanja wa ndege.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kwenye nchi ya Kuwait na Tanzania. (Wa kwanza kushoto) ni Mhe. Prof. Abdillah Omari, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait mwenye makazi yake Saudi Arabia na (kulia) ni Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Najib na kuangalia picha za viongozi mbalimbali wa Kuwait.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...