Tamasha la ZIFF limetangaza filamu 16 zitakazoshindana katika kugombea tuzo ya Sembene Ousmane katika tamasha litakalofanyika baadaye mwaka huu. Filamu zinatoka katika nchi 11 ambazo ni pamoja na Marekani, Brazil, Senegal, Madagascar, Ghana, Cameroon, Morocco, Kenya, South Africa, Ethiopia and Tanzania.


“Shindano hili limetungwa ili kuboresha ufundi wa kutengeneza filamu fupi zinazobuniwa nna vijana wa Kiafrika”, alisema Fabrizio Colombo, Mkurugenzi Msaidizi wa ZIFF. “Filamu 16 zimo katika kinyang’anyiro hicho, na washindi watatu watapewa $2000 kila mmoja ili kuwasaidia kutengeneza filamu nyingine tayari kwa tamasha la ZIFF mwaka ujao” aliongezea.

Bernd Multhaup wa shirika la GIZ, wadhamini wa tuzo hii, alinakiliwa akisema, “Tuliamuwa kutoa zawadi tatu ili kuwapa motisha watengeneza filamu wengi zaidi kwa kupitia tuzo ya Sembene. Tunatambuwa kuwa filamu fupi zinauwezo mkubwa wa kuboresha ubunifu bila ya kupunguza ubora wa filamu”.

Hao washindi watatu watatakiwa kutuma hadithi zao pamoja na mpango-kazi wa utengenezaji wa hizo filamu kabla hawajapewa fedha walizoshinda ili kuhakikisha filamu zitatengenezwa kuwahi tamasha lijalo mwakani. Kwa njia hiyo ZIFF itahakikisha kupata filamu nyingine na kuboresha ufundi wa kutengeneza filamu fupi na bora.



Filamu 16 zilizochaguliwa ni:

Lesley: Victor Okoye Frank, USA / 15 min
O Canto da Iona: Thiago B. Mendonca, Brazil / 25 min
Maruna: Molly Kane, Senegal / 15 min
Aisaa’s Story: Iquo B Essien, USA / 15 min
Madama Esther: Luck Razanajaona, Madagascar / 15 min
The Traveller: Victoria Dogbe, Ghana / 9 min
Damaru: Agbor Obed, Cameroon / 24 min
Houkak: Younes Youfsi, Morocco / 17 min
Kwaku: Anthony Nti, Ghana / 16 min
Samaki Mchangani: Amil Shivji, Tanzania, 30min
Kilimo 2: Neema & Warren Reed, Tanzania / 6 min
Liberte Emprisonnee: Sara Mikayel, Senegal /16min 
Soko Sonko: Ekwa Msangi, Kenya / 22 min
Uthando: Tulanana Bohela, South Africa, 20min
Grandma Knows Best: Tamara Dawit, Ethiopia, 16min
Vitrin, Regis Talia, Cameroon, 15min
----------------------------------------------------------------------------------
Juu Ya Mradi: Mradi huu unadhaminiwa na GIZ, shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani  ambalo linasaidia Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki. ZIFF ni tamasha kubwa kuliko yote Afrika mashariki na ambalo linatambuliwa kimataifa. Tamasha linadhaminiwa na ZUKU kupitia mkataba wa udhamini wa miaka 10 utaoisha 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...