Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.                                                           
Naibu waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mahamoud Thabiti Kombo amesema bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi inajenga maabara ya kisasa  ya uchunguzi wa madawa , chakula na vipodozi ambayo itakuwa na ubora wa Kimataifa.

Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashimu Ayoub aliyetaka kujua kwamba bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi ni taasisi muhimu kwa afya za binaadamu, kwanini Wizara haifikirii kuipa ruzuku na lini watawapa ruzuku hizo.

Alisema ruzuku  ya bodi hiyo itapatiwa katika bajeti ijayo na zaidi ya  milioni 70 zimetengwa kuipa bodi hiyo ili kuyafikia mahitaji yao  ikiwa pamoja na ujenzi huo wa maabara.“Hivi sasa bodi wana tengeneza laborali ya kisasa inayoweza ushindani kuvipima vyakula vinavyoingia nchini”,alisema Naibu Waziri huyo.

Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa hakuna ruhusa ya chakula, dawa na vipodozi kuingia dukani bila ya bodi hiyo kuvifanyia uchunguzi wa kimaabara na pale vitu hivyo vinapobainika kuwa ni vibovu ndio bodi huchukua jukumu la kuviangamiza.“Inapobainika kuwa chakula, Madawa na vipodozi ni vibovu basi mmiliki hupigwa faini kwanza na baadae hulazimika alipie kazi ya uangamizaji”, alisema Mahamoud.

Wakati huo Naibu Waziri huyo kwa niaba ya Waziri wa Afya alitoa tarifa fupi ya dharura juu ya ukosekanaji wa maji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ambayo ilileta usumbufu mkubwa hospitalini hapo.Hata hivyo alisema huduma hiyo tayari imeshapatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano na mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ambapo huduma hiyo  inapatikana bila ya usumbufu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...