Afisa mwandamizi wa Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawiche akikabidhi mfano wa hundi ya sh laki sita kwa Sue Hurford ambaye mbuzi wao aliibuka kidedea wa shindano lililopewa jina la CBA ‘Sparkers’ lililodhaminiwa na benki hiyo wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Fedha hiyo itapewa Hospitali ya CCBRT.
Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano katika mbio za mbuzilililopewa jina la 'CBA Sparkers’ lililodhaminiwa na benki ya CBA wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa mwandamizi wa Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawiche akionyesha cheti alichokabidhiwa kutokana na benki ya CBA kudhamini mashindano hayo ya kuchangia fedha za kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji maalum katika jamii wengine pichani ni wafanyakazi wenzake na waandaaji wa shindano hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...