Na Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amewataka viongozi wa Tarafa ya Dodoma mjini kuwaelimisha wananchi wanaowaongoza na wanaofanya kazi chini yao juu ya matishio na viashilia vya uvunjifu wa sheria na amani ili wote waweze kuwa na uelewa wa pamoja kuvibaini, kuvizuia na kuvitolea taarifa kwa vyombo vya dola waweze kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Ameyasema hayo wakati akitoa elimu juu ya hali ya ulinzi na usalama na matishio ya kiuhalifu katika kikao kilichojumuisha wakuu wa vyombo vya dola Mkoa wa Dodoma, Uongozi wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Katibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa, Viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Baraza la wazee Dodoma, Mwenyekiti wa TCCIA, Mameneja wa Hoteli mbalimbali, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali na Wazee maarufu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP David Misime akitoa elimu katika mkutano huo.
Kamanda MISIME amewataka kila mmoja kujiuliza kama eneo lake analoliongoza au kama kiongozi wa familia je eneolake linausalama wa kutosha? Je sio eneo ambalo wahalifu wanaweza kuligeuza kuwa maficho ya kuandalia mikakati ya kutekeleza matendo yao ya kiuhalifu?
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...