Katibu Mkuu wa Sirika la Dawa Asili na Ulizi wa Mazingira Boniventure Mwalongo akifafanuaa jambo mbele ya waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusiana na Maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Leo katikati ni Mwenyekita wa Chama Cha Albino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe na Katibu Mkuu Ziada Nsembo.
Katibu Mkuu wa TAS, Ziada Nsembo akizungumza na waandishi wa habari Hawapo pichani katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo,kushoto ni Mwenyekita wa Chama Cha Albino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia kwenye Mkutno  wa TAS  jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Idara Habari MAELEZO. PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino ambayo yameandaliwa na Chama Cha Albino Tanzania yatayofanyika Juni 13 mwaka huu  jijini Arusha.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekita wa Chama Cha Albino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.

Kirwe, amesema kuwa  maadhimisho hayo yana lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kuwa ni watu wa kawaida kasoro yao ni upungufu wa baadhi ya seli zinazosaidia kutengeneza rangi ya ngozi tuu na sio kitu kingine.

Ameongeza kuwa watu wenye ualbino  ukiwaua au kukata viongo vyao huo ni upotofu wa imani tuu na ni imani za kishirikina  inatakiwa kuepukana na tabia ambazo hazituletei faida yoyote.

Nae Katibu Mkuu wa TAS, Ziada Nsembo amesema kuwa nchi zitakazo shiriki katika  maadhimisho hayo  ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda Malawi, Uingereza,Marekani na Swideni pia nchi nyingine zinaendelea kujiandikisha ili kuungana ili kutokomeza na kutoa Elimu juu ya watu wenye ualbino.

 Maadhimisho hayo hapa nchini yanaratibiwa na Chama Cha Albino Tanzania (TAS),Serikali chini ya Ustawi wa Jamii,Jukwaa la Tiba Asili Tanzania shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania New hope Family, Upendo Daima, Shirika la Dawa Asili na Ulizi wa Mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...