Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
1.     Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
2.     Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
3.     Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
4.     Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
5.     Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015 na;
Tumaini Makene

Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...