Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani ya kipindi cha miaka 10 huku asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa.
Asilimia hiyo inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda Mlima huo kwa muda wa siku moja hali inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi zetu ili kujionea urithi tuliopewa na Mungu.
Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema katika kuhamasiosha utalii wa ndani ,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu na mlima kuweza kuupanda kwa muda wa siku moja na kurudi.
.jpg)
Mhifadhi utalii katka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akizungumza juu ya ofa iliyotangazwa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima huo kwa siku moja na kurudi hadi kilele cha Shira.
.jpg)
Afisa masoko wa KINAPA ,Antypas Mgungusi akisistiza jambo wakati akizungumzia juu ya ofa ya safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku akishauri wenye sherehe zao kutumia nafasi hiyo kupanda Mlima huo kwa ajili ya kufanya sherehe zao,alitaja sherehe ambazo zinaweza fanyika katika hifadhi hiyo ni pamoja na wale wenye kukumbuka siku zao za kuzaliwa wanaweza fanya hivyo wakiwa kileleni,lakini pia kwa wale wanaoenda Honey Moon baada ya ndoa pia wameshauriwa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha ofa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...