Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2015

    hongera sana mh. rais JK kwa kusema ukweli mtupu bila kumung'unya maneno, umenikumbusha bb wa taifa pia alivyokua anatoa makavu live.Muhimu walengwa waelewe watanzania wa leo sio wa jana kwahio sio ajabu hata CCM kinaweza pigwa chini pia.. big up JK.
    mdau wa Oxford, UK

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2015

    Kama CCM inatuletea mjombea msafi mwenye historia nzuri ndani na nje ya chama kutampa kura zetu. Lakini wale wanaotafuta umaarufu kwa pesa na makundi hatuwataki. CCM chagueni kusuka au kunyoa. Hogopeni siasa za Urafiki na upendeleo. Chagueni mtu msafi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2015

    Unajua bwana Mh Rais Kikwete ni bonge la Rais ambae ni hazina ya nchi yetu nina mfatilia sana na kila mara naziona hekima zake na ametoa onyo kwa wale wote wanaotaka kuonesha ubinafsi wa kulazimisha ndoto zao za kuwa Rais wakati ni Wachafu...Sasa waachie ngazi na waonesha uzalendo kwa Chama na Taifa sababu sio lazima wote tuwe Rais.

    Big up JK, Big Up sana Rais wangu kwa hekima zako na maono yako.

    Msg sent and derivered!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2015

    Mimi sina chama, Sina ukabila wala sina udini ila nina Utaifa ambao ndio chama changu, ndio kabila langu na dini yangu...

    Nimekaa nje ya nchi zilizoendelea zaidi ya miaka 7 na sijawahi ata siku moja kumuona Mwanasiasa yoyote akitumia mamilioni au mabilion ya Pesa eidha akiusaka Urais au Uwaziri mkuu ktk hayo mataifa ila ukija Tanzania utashangaa kuona watu wanamwaga pesa waziwazi kununua vyeo!!

    Sasa nikiwa kama Mtanzania najiuliza anayetoa hizi pesa zote anategemea akiupata Urais?? Nabaki namuogopa sana!! Najiuliza tena je kwa vile anaupenda Urais, akiupata ataweza kuachia ngazi baada ya muda wake?? Nabaki namuogopa Sana!!

    Naombeni nyie wanaCCM Msikilizeni sana Mh Rais JK msije mkajuta hapo baadae akiondoka...Leo hii tunalia sana kwakuwa JK mwingine mtoa maono hayupo!

    Nakuomba Rais wangu kwa niaba ya Taifa na watoto wetu hakikisha atakae kuwa Rais atakuwa ni mtu Msafi na wala hasinunue Urais kama bidhaa kwa maana Ikulu ni mahali patakatifu!!

    Long live JK

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2015

    Nadhani hapo Hon. JK atakuwa amenawa! Ni ukweli kuwa watakao chagua Mgombea wa Uraisi hatimaye watakuwa ni wajumbe wa vikao vinavyohusika lakini ni muhimu sana Hotuba ya Mwenyekiti itoe muelekeo wa hatima ya Chama hasa ikiwa Wajumbe watakaidi maonyo hayo ya Mwenyekiti...Historia itawahukumu wajumbe ikiwa baada ya Hotuba na maelekezo kama hayo eti watajifanya hawaelewi na bado wataendekeza makundi na Ubinafsi usio na tija kwa Chama (CCM) na hata kwa Taifa ila kwavile tu mtu fulani ameapa lazima apitishwe, hapan isiwe hivi. Ni muhimu kujua kuwa ikiwa mgombea fulani ni chaguo la watu atapita tu hakuna haja kutumia nguvu kubwa sana. Ukitumia nguvu kubwa unawaogopesha unaotaka wakuchague maana watahoji nini msukumo huu nyuma ya kuutaka U-President, Je ni Uzalendo au Ubinafsi? Hongera Hon. JK - Umeweka wazi kazi kwa Wajumbe sasa!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2015

    Ah, wapi bwana. CCM waoga na watamchagua mtu kwa kumwogopa kwamba wamemlia hela yake atawafanya vibaya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2015

    Maneno mazito zaidi aliyatoa Mwalimu Nyerere kuhusu hilo! Je walimsikiliza? Tatizo mi nafikiri ni sisi wotawaliwa, kwa sababu kuna nguvu ya ziada inayomchafua yeyote atakayeingia Ikulu kwa matakwa yao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...