Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Madereva wamepewa kipaumbele  kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani tume hiyo itakuwa na wajumbe watano  kutoka  Umoja wa madereva tuu na kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu .

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.

Makonda amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na  uchaguzi wa madereva wenyewe pia  na wajumbe wengine watatoka  Mamlaka ya usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na mambo ya ndani.

Makonda ameongezea kuwa Mgomo wa madereva hautakuwepo tena milele, madereva wachague wajumbe  ambao wanaweza kuhakikisha haki zao kinasimamiwa vizuri na kutatua matatizo yao.

Tume hiyo itaanza kufanya  vikao vyake ijumaa ya wiki hii.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano wa wandhi wa habari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MsemaKweliMay 08, 2015

    huyu mkuu wa wilaya kanyoa kiduku?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...