1.USHAHIDI WA
KUAMBIWA NI NINI?
Ushahidi wa kuambiwa
ni ushahidi unaotolewa
na mtu ambaye
hakuona tukio likitendeka,
hakusikia tukio likitendeka,
hakuhisi wala kuonja, wala
kunusa jambo lililo mbele
ya mahakama kama
kosa isipokuwa aliambiwa
na mtu mwingine aliyeona, kusikia, kuhisi, kunusa au
kuonja.
Hapa kuna
watu wawili, kwanza
aliyeona au kusikia , na
pili yule aliyeambiwa
na huyu aliyeona
au kusikia . Kwahiyo
katika maana yetu huyu
wa pili
aliyeambiwa na wa
kwanza aliyeona au
kusikia ndiye mwenye
ushahidi wa kuambiwa. Ni
kwa maana hii tunasema
huyu wa pili
aliyeambiwa akienda kutoa
ushahidi wake mahakamani
utaitwa ushahidi wa
kuambiwa.
Kwa mfano “A” amemuona “ B”
akimuua “C”. “ A”
baada ya kuona
tukio lile akamwambia
rafiki yake “D”. Ina maana “D” hakuona
lolote isipokuwa ameambiwa
na rafiki yake “A” aliyeona. Kwa
maana hii ushahidi
wa “D” ni ushahidi
wa kuambiwa. Ameambiwa
na nani, ameambiwa
na “A” aliyeona
tukio. Hii ndio
maana ya ushahidi wa
kuambiwa. Kwa jina
la kitaalam ushahidi
huu huitwa “hearsay evidence” .
Na kwa jina
jingine la mtaani
huitwa “ ushahidi wa nilimsikia
akisema”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...