Na Bashir Yakub.
Siku zote wananchi wamekuwa wakililalamikia jeshi la polisi kwa namna linavyoendesha shughuli zake hasa wakati wa ukamataji (arrest). Matumizi ya nguvu, ubabe na kutofuata sheria na taratibu maalum limekuwa ndio tatizo kubwa kwa wananchi dhidi ya askari.
Sio siri askari wamekuwa wakitumia nguvu na ubabe mno katika kuwakamata raia. Hata pale pasipo na haja yoyote ya kutumia nguvu bado wao wamekuwa wakilazimisha nguvu nyingi hali ambayo hupelekea vurugu , kuumizana na hata mauaji. Mara nyingi unapochunguza matukio mbalimbali ya vurugu ambayo huwahusisha raia na polisi utagundua kwa haraka kuwa ubabe wa askari ndio uliopelekea vurugu. Basi leo nitaeleza nini ufanye askari anapokiuka taratibu hasa wakati wa kukamata/kuweka chini ya ulinzi.
1.NINI MAANA YA KUKAMATA ( ARREST ).
Sura ya 20 Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho 2002 ndiyo sheria inayotoa mwongozo wa namna na jinsi ya kumkamata mtu. Pamoja na hayo sheria hii haikueleza moja kwa moja nini maana ya kukamata. Hata hivyo kutokana na miongozo mbalimbali ya kimahakama ambayo hutumika kutafsiri sheria hii tunaweza kupata tafsiri ya neno kukamatwa kwa kusema kuwa ni tendo la kumzuia kwa muda raia ambaye inatuhumiwa kwa kosa fulani, ambalo hufanywa na mamlaka husika.
Kwa tafsiri hiyo tendo la kuzuia lazima liwe la muda, raia anayekamatwa lazima awe ametuhumiwa, na pia ukamataji lazima ufanywe na mamlaka. Huo ndio utakuwa ukamataji ( arrest).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...