Na  Bashir  Yakub.

Malalamiko  ya raia  dhidi  ya  jeshi  la  polisi  hayataishi  kama  polisi  wenyewe hawatajirekebisha.  Na ieleweke kuwa  si  kweli  kwamba wanaolalamika  ni  wajinga  au hawana sababu  za  msingi.  Mara  zote  ukiangalia  malalamiko  ya  raia huwa  ni  ya  msingi  na  mzizi  wake ni  mmoja  tu.  Ni  utamaduni  wa  askari  wetu  kutopenda  kutenda  hatua  kwa  hatua  kama sheria  inavyoagiza. Sheria  imetoa  maelezo  mazuri  tu  ya namna  ya  kuyaendea  mambo. Tatizo  watekelezaji  ndio  hakuna. 

 Sheria  husema  kingine  na  watekelezaji  hufanya  kingine. Namna  hii  huwezi  kuepuka  chuki  na  migongano  kati  ya   hawa  watekelezaji  askari  na  raia. Na  migongano  na  kutokuelewana  kunapokuwa  kukubwa  na  usalama  nao  unayumba  kwakuwa   ili  askari  afanye  kazi  ya  usalama  vizuri   anategemea  msaada  wa  raia  karibia  kwa  asilimia  zaidi  ya  80.  '

 Na  raia  huyu hatatoa  ushirikiano  wakati  jana  umempiga  bila  sababu,  umemtukana   na  kumtolea  maneno  ya  kebehi. Makala  iliyopita  nilizumgumzia  namna  sheria  inavyomruhusu  raia  kukataa  kukamatwa  na  polisi  iwapo  polisi  huyo  atakiuka  taratibu  katika  ukamataji.  Leo  nazungumzia   namna  sheria  inavyokataza kumchukua  mtu  mwingine  baada  ya  kumkosa  mtuhumiwa  halisi  wa  kosa.  Tutaona  hili  likoje. 

1.ASKARI  KUONDOKA  NA  MTU  MWINGINE  BAADA  YA  KUMKOSA  MTUHUMIWA  HALISI.

Hii  ni  tabia  ambayo  imezoeleka  sana  na  ipo  kwa  muda  mrefu. Yumkini  kuzoeleka  kwake  na  kuwepo  kwake  kwa muda  mrefu hakuifanyi  hata  kwa  sekunde  moja  tabia  hii  kuwa  halali  kisheria.  Mara  nyingi  wanaokutwa sana  na tabia  hii  ni  watu  wa  vijijini  hasa  wa  hali  ya  chini.  Lakini  hata  mijini  pia  ipo  sana.  Nazungumzia   tabia  ya  kuondoka  na  mtu   mwingine  baada  ya  kumkosa mtuhumiwa  halisi.  Kwa  mfano  askari  wamekuja  nyumbani  kumtafuta  JOHN  kwa  kosa  analotuhumiwa  nalo.  Bahati  mbaya  au  nzuri  JOHN  hayupo  nyumbani. 

Kutokana  na hilo   askari  wanaamua  kuondoka  na  mke  wa  JOHN  au  mtoto  wake     ili  kumfanya  JOHN  aweze  kutokea. Hiki  ndicho  ninachozungumzia.  Na wanaokuwa  wakichukuliwa  mara  kwa  mara ni  mke  wa  mtuhumiwa  , mtoto  au  ndugu. Lengo   eti  ni kumfanya  mtuhumiwa  halisi  aweze  kujisalimisha. 

SOMA HAPA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...