Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos makalla jana amehutubia maelfu ya wananchi wa mji Mdogo wa madizini na Vijiji vya jirani  huku akikabidhi Fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa vikundi 12 na mabati 200 yenye thamani ya shilingi milioni Tatu kwa ajili ya kupaua Jengo la Tawi la CCM madizini bati 100, misikiti wa lusanga road bati 50 na kanisa la full salvation church bati 50.

Akihutubia maelfu ya wananchi hao aliwaeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake amekuwa ni mdau mkubwa wa kusaidia vikundi, makanisa, misikiti na shughuli nyingi za maendeleo na amewatadharisha wanaotamani jimbo la Mvomero wajipime kama wanaweza kwani kwa umati huu na matamko yanayotolewa na Makundi mbalimbali jimboni ni dhahiri wanaotaka jimbo la Mvomero ni sawa na mtu anayesubiri Ndege bandarini.
Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa mji Mdogo wa madizini, Mvomero.

Akikabidhi misaada hiyo alisema ameamua kujibu barua za maombi ya vikundi vya ujasiriamali vya Vijana na akinamama vya vitongoji Sita vya madizini na vikundi viwili vya kijiji cha kichangani. Vikundi vilivyofaidika na msaada huo ni mji mpya,kibaite,mpingoni,Kkkt,barabarani,madizini B,kiwandani, Gezaulole, kazi kwanza,Vijana mpingoni , ushonaji kichangani na soko la ndizi kila kikundi kilipata shilingi laki tano.

Alivipongeza vikundi kwa shughuli wanazifanya na akawataka wengine kuiga mfano huo kwani umoja ni ushindi. Aliwaahidi ataendelea kuwaunga Mkono kwani katika kipindi chote cha uongozi wake amesaidia vikundi vingi jimboni.
Kuhusu kero ya kucheleweshewa malipo ya miwa na mishahara kwa wakulima na wafanyakazi wa kiwanda cha Mtibwa ameeleza hatua alizochukua ikiwemo kuipeleka Kamati ya viongozi wa wafanyakazi na wakulima kuonana na Waziri mkuu na jambo hilo linashughulikiwa na hata hivyo katika hatua ya awali amewajulisha ujio wa Waziri wa kilimo na Chakula, Steven Wasira atatembelea kiwanda na kuongea na menejimenti ya kiwanda, wafanyakazi, wakulima na wananchi jumatatu tarehe 25 mei.

Amewaomba wawe watulivu wakati huu ambao ofisi ya Waziri mkuu na wizara ya kilimo ikishughulikia tatizo hilo

Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos makalla akikabidhi mabati kwa viongozi wa Dini katika mji Mdogo wa madizini, Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...