Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden Kinondoni unapitisha wikiendi bila burudani yoyote na badala yake onyesho la Yamoto Band na Mashauzi Classic leo usiku ndio show pekee wiki hii katika ukumbi huo. 

Kesho Ijumaa  Malaika Band ambao hupiga hapo Mango kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini. Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.

Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la nyama choma.

Yamoto Band watakwea jukwaa la Mango Garden Kinondoni leo usiku (Alhamisi, 28) kuonyeshana kazi na wenyeji wao Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi.

Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...