Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernet Mangu  akimpa mkono mshindi wa  Kwanza wa Riadha  ya Half May Day Marathon katika kundi la Wanaume,Alphonce Felix wa Club ya Holili,Kilimanjaro yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Boa  Bank Ammish Owusu, mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
.Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa  Kwanza  wa  Riadha ya   Half May Day Marathon katika kundi la wanawake,Natalie Elisante Arusha) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Suleiman Kova ,mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa Pili  wa  Riadha ya Half  May Day Marathon katika kundi la wanaume ,Joseph Panga (Arusha) yaliyofanyika leo katika viwanja Polisi Ostebay jijini Dar es Salaam wanaoshuhudia ni ,Mkurugenzi wa Benki ya Boa,Ammish Owusu .

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu  amesema michezo inajenga ukakamavu wa mwili hivyo kwa washiriki wa may day marathon wamefanyoa  afya.

Mangu ameyasema aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati  mashindano ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam ,aliwapongeza washindi na kutaka waongeze juhudi ili waweze kufika mbali katika mchezo wa riadha.  Washindi wa May Marathon wamepongeza waandaji wa mashindano hayo kwani yanaongeza chachu ya kupenda mchezo huo.

Washindi hao wameyasema hayo katika mashindano  ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterba jijini Dar es Salaam ,wamesema kuwa mashindano hayo yameamsha kupenda mchezo wa riadha kuendelea kupendwa.

Akizungumza  na mshindi wa kwanza katika upande wa wanaume ,Alphonce Felix amesema ameshinda katika mashindano hayo kwani alijituma kutokana na mazoezi ya mara kwa mara na kuwataka watu wengine kushiriki mchezo huo kutokana na kujenga afya zao.

Amesema riadha ni mchezo mmoja mzuri kutokana na utaratibu kujpangia mazoezi  kwa ni riadhia ni ajira kama michezo mingine.

Mshindi wa Kwanza  kwa upande wa Wanawake ,Natalie Elisante (Arusha)amesema amewataka wasichana kushiriki katika riadha mbalimbali kwani wasichana na wanawake wanaoshiriki mchezo huo ni wachache ikilinganishwa na idadi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...