Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msahuri,kumbukumbu za ukombozi wa Barani Afrika,Daniel Ndagala, Mshauri na mtafiti UNESCO Phelippe Roisse na wa mwisho ni Dinah Mumbaga Mtafiti na mshauri wa UNESCO.(Picha na Avila Kakingo).
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Ukombozi Barani Afrika, maadhimisho hayo yatazinduliwa katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Mei 25 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maadhimisho hayo ya wiki ya Ukombozi Barani Afrika.
Mwambene amesema kuwa Serikali ikishirikiana na shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watazindua Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania(TAHAP), ambao ukikamilika utakuwa unaweka na kutunza kumbukumbu za nyaraka mbalimbali zinazohusu Ukombozi Barani Afrika.
Amesema kuwa miongoni mwa matukio muhimu katika maadhimisho hayo ni pamoja na mdahalo unahohusu mchango wa vyama vya siasa katika harakati za ukombozi utakaoongozwa na Dk. Salim Ahmed Salim, Profesa Issa Shivji pamoja na Mh.Ibrahim Kaduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...