Viongozi wanaounda Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili wametakiwa kusimamia vizuri tathimini ya utendaji ulio wa wazi kwa wafanyakazi walioko chini ya Kurugenzi, Idara na Vitengo wanavyoviongoza ili kuleta tija mahali pa kazi. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto wakati alipokuwa akizindua semina ya siku nne kwa viongozi hawa iliyoanza leo, jijini Dar Es Salaam ambapo mada kuu ni jinsi ya kusimamia vizuri tathimini ya utendaji ulio wa wazi (OPRAS) kwa wafanyakazi.

“Nataka kuona mabadiliko kwenye tathimini za wafanyakazi walioko chini yenu katika kipindi cha mwaka wa fedha unaolekea kuisha Juni mwaka huu zikiwa zimejazwa vizuri, shirikishi na zenye kutoa alama zinazotenda haki kwa mfanyakazi na mwajiri” amesisitiza Dkt. Kidanto.

Sitapenda kusikia malalamiko yasiyo na msingi kwa kiongozi ambaye anamlalamikia mfanyakazi fulani kwamba hafanyi kazi yake vizuri alafu mwisho wa mwaka anampa alama za juu, amesema Dkt. Kidanto.“Viongozi acheni kuwajazia maksi  za juu na kupendekeza kuwapandisha vyeo wafanyakazi walioko chini yenu ambao hawatimizi wajibu wao” amesema Dkt. Kidanto.  

Semina hii ni ya siku nne inayoendeshwa na wataalam wa Menejimenti kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Mada nyingine zitakazofundishwa ni pamoja na uhusiano uliopo katika ya mifumo ya usimamizi wa Utendaji na  tathimini ya utendaji ulio wa wazi, na mkataba wa huduma wa wateja, changamoto katika utekelezaji wa tathimini ya utendaji ulio wa wazi, ufahamu wake, malengo ya kimkakati yaliyokusudiwa,  uhalisia wa malengo ya mpango mkakati, suala la tathimini ya utendaji ulio wa wazi kuwa ni matakwa ya kisheria  na namna ya kutoa taarifa.

Mada hizi zinatolewa na Prof. Josephat Itika ambaye in Bingwa wa Masuala ya Menejimenti na Utawala, Prof. Joseph Kuzilwa ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambayeni mtalaam wa masuala ya tathimini ya utendaji ulio wa wazi na Pro. Faustin Kamuzora ambaye pia ni Bingwa wa Masuala ya Menejimenti.
Aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akifungia semina ya Viongozi wa Menejimenti ya Hospitali juu tathimini ya utendaji ulio wa wazi. Kushoto kwake ni Prof. Josephat Itika ambaye ni mwezeshaji na Bingwa wa Masuala ya Menejimenti na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Prof. Itika akitoa mada kwa washiriki wa hiyo ambao ni Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Mameneja wa Majengo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa MNH wakimsikiliza kwa makni mtoa mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...