Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.

Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.

Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities).

Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).

Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.

Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.

Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2015

    HONGERA SANA MKUU, NA WENGINE WAJIFUNZE KWAKO MAVITU GANI UNAFANYA, SIO WANAENDA TU WAKIVURUGAVURUGA HAPA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2015

    Nini vigezo vya kumpata meya bora Africa?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2015

    Hongera kwa ushindi huu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2015

    vigezo mmh! Meya tunaonmba ufanye kazi tuzo sisi havitusaidii ikiwa hali ni mbaya. Pesa hizo zisiende kwenye uchaguzi bali zitumike kuboresha Kinondoni Municipal kwa upande wa hospital ya M/nyamala ni zerooo!!! aibu tupu kuliko kulazwa pale bora ulale home dr aje akutibia!!! barabara ndio usiseme hayo maeneo ya M/nyamala sokoni, Hombus, Kijitonyama mnapelekaje daladala bila kutengeneza miundo mbinu ya barabara, Sinza ni zaidi ya swimming pools.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...