Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva nchini, Rashid Saleh akiwatuliza madereva wenzake wakati wakiusubiri Uongozi wa juu wa Serikali waliotaka kuzungumza nao juu ya matakwa yao waliyoomba wafanyiwe, pindi walipokutana na Serikali majuma kadhaa yaliyopita.
Madereva na mabango
Baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani wakiwa nje ya ofisi yao wakiwasikiliza viongozi wao (hawapo pichani).
Askari wa  Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam asubuhi ya leo kusimamia  usalama kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi ulioanza leo kwa mara nyingine kushinikiza kutekelezewa matakwa yao 
Mabasi yanayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na mikoa ya kusini yakiwa yameegeshwa kwenye kituo cha Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam katika mgomo wa madereva  leo Hadi muda huu hakuna basi lililoanza safari kutokea kituoni hapo.
Kituo cha Daladala cha Mbagala Rangi Tatu kikiwa kimefurika abiria kufuatia mgomo unaoendelea.

Habari na picha zaidi zitawajia baadae kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...