Mgomo wa Madereva uliodumu kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata muafaka baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (pichani) kufanikiwa kuusuluhisha kwa kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva.
Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha Mikataba kwa Madereva, malipo kwa madereva hao, pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao, na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu.
Akizungumza na Madereva hao, Mhe, Makonda amewataka Madereva hao kuachana na mgomo huo na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyika kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho.
Aidha, Mhe Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa, ambayo itajadili masuala ya Mkataba, malipo, matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.
Pia Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini Dar es Salaam.
Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva, Bw. Rashidi Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA HALI ILIVYOKUWA
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA HALI ILIVYOKUWA
Duh!.hivi mkuu wa wilaya anayo mamlaka ya kuliambia jeshi la polisi kumwachia mtu aliyevunja sheria? Si Tz mnafata sheria na utawala bora?siamini khaa!!
ReplyDeleteSipati picha ikitokea hapa marekani sijui watu wagome/waandamane kutetea uhalifu halafu rais ..aje aseme waachiwe huru?kwa maneno???duh.!kweli bongo Tambararee!
mdau
Washington DC
Afadhali suluhisho hili ni afueni kwa wasafiri.
ReplyDeleteKatika conflict mitigation hiyo ni possible. Wanaachiwa kumaliza tatizo. Ni common practice sehemu nyingi duniani
ReplyDeleteSielewi unaposema serikali iboreshe mikataba ya madereva, na malipo yao. Kwani mwajiri wao ni serikali?!
ReplyDeletemweee! wadau munaochangia kwa kuongea na kiingereza na kuswahili munatuacha njia oanda khaaa! . Ongeeni lugha moja ilituwaelewe basi moja kwa moja sio munatuchanganyia lugha. asante. Mimi Andrew Chale Tanzania.
ReplyDelete