Na Bashir Yakub.
Ni jambo la kutia faraja kuwa vijana wengi wamekuwa wajasiriamali na wanafanya biashara mbambali katika maeneo mbalimbali ya nchi. Wengine biashara ni nzuri na wengine wanalalamika biashara sio nzuri. Kila mtu ana muono wake kuhusu mwenendo wa biashara zake.
Pamoja na hayo ushahidi wa sayansi ya biashara unathibitisha kuwa kwa asilimia zaidi ya 70 suala la biashara kuwa mbaya au nzuri hutokana na mtu mwenyewe alivyojipanga. Mbinu, umakini, mtaji, uendeshaji, mipango, na weledi. Nilipoandika kuhusu njia au namna ya kuunda kampuni nilieleza kuwa masuala ya uendeshaji wa kampuni huwa ni masuala ya kisheria. Kila kitu katika kampuni ni sheria kuanzia usajili, uendeshaji mpaka kufa kwa kampuni .
Ni kwa maana hii nasema kuwa mjasiriamali anapopata ushauri mzuri wa masuala mbalimbali ya sheria katika uendeshaji wa kampuni basi yaweza kuwa nafasi ya ustawi wa kampuni. Leo nazungumzia kitu kingine cha kisheria katika uendeshaji kampuni kiitwacho mikataba kabla ya kampuni ( pre incorporation contracts). Tutaona hapa chini maana na umuhimu wa kujua kitu hiki.
1.NINI MAANA YA MIKATABA KABLA YA KAMPUNI ( PRE INCORPORATION CONTRACTS ).
Mikataba kabla ya kampuni ni kama jina lenyewe linavyojieleza. Hii hujumuisha biashara alizokuwa anafanya mtu kabla ya kuwa na kampuni lakini baadae akawa na kampuni na akaendeleza biashara zilezile. Watu wengi ambao tayari wameanzisha makampuni hujikuta walikuwa na biashara zao hata kabla ya kuunda makampuni hayo. Pengine kutokana na biashara kupanuka mtu anaamua kuunda kampuni ili kuendeleza biashara ileile. Kwa ufupi maana ya hili ni kuwa, ni ile biashara aliyokuwa nayo mtu na kuamua kuiundia kampuni .
Mtego ( technique) wa kisheria uliopo hapa ni kuwa umekuwa na biashara ambayo haikuwa kampuni , ina maana katika biashara hiyo umefanya mikataba mbalimbali kwa mfano umefanya mkataba wa pango au mkataba wa manunuzi ya eneo la biashara, umekuwa ukinunua bidhaa mbalimbali kwa kuandikishana au kupewa risiti( risiti nayo ni mkataba),mikopo mbalimbali, ulinunua mali mbalimbali kwa ajili ya biashara zako kwa mfano gari, pikipiki, baiskeli au maguta kwa ajili ya kubebea mizigo n.k Hii yote ni mikataba uliyoifanya kabla ya kuunda kampuni na ndio huitwa “pre incorporation contract”.
Swali ni je utakapounda kampuni na biashara hiyo yote na mali zake kuziweka chini ya kampuni , mikataba hiyo itakuwa inaibana kampuni na je kampuni inawajibika kwa lolote litakalotokana na mikataba ambayo imeingiwa kabla ya kuundwa/kuzaliwa kwake ?.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...