Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kujadili na kufanya uamuzi wa kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi katika wilaya ya Sumbawanga na Kalambo leo tarehe 23 Mei 2015. Kikao hicho kimeridhia mapendekezo hayo ya Halmashauuri husika baada ya kukidhi vigezo ambapo yatapelekwa ngazi za juu kwa uamiuzi zaidi. 

Majimbo hayo yatazaliwa katika majimbo yaliyopo hivi sasa ambapo kwa jimbo la Kwela ambalo lipo katika Wilaya ya Sumbawanga litazaa jimbo la Ziwa Rukwa baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ikiwemo ya idadi ya watu na ukubwa wa jografia. Kwa upande wa jimbo la Kalambo ambalo lipo katika Wilaya ya Kalambo linatarajiwa kuzaa Jimbo jingine la Mambwe. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa taarifa iliyopokelewa na ofisi yake kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya maelekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni muwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...