Mwanamuziki mkongwe na mtunzi Tshimanga Kalala Assosa

​UZINDUZI WA KITABU NA KAVASHA CLUB...
Jumapili hii tarehe 03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa atazindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.
Ni kitabu cha "Jifunze LINGALA kwa Kiswahili".
Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).
Ni ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi saa 3 jioni. MRC ndio ukumbi ambao "Club Raha Leo Show" ya TBC1 ilikuwa inafanyikia.
Tshimanga Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis.
Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.
Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2015

    The mdudu, Lingala ndani ya Tanzania? Kama hamna kazi za kufanya ni bora mtumie muda huo kutembelea wagonjwa ili muwape faraja na kuna watoto yatima pia kwenye vituo vya kuwalelea mwende huko pia.....achaneni na mambo ya kijinga janga yasio na tija na katika hao wanao kisubiri mimi simo kabisa

    ReplyDelete
  2. Ankal

    Shukrani kwa taarifa hii. Nikizingatia ukaribu ulioko baina ya watu wa DRC na sisi, mahusiano yaliyopo katika biashara, utamaduni, na kadhalika, lugha ya Lingala ni kiungo kinachoweza kufungua milango mingi.

    Nitakitafuta kitabu hiki. Nategemea mtungaji au mchapishaji ataeleza kinapatikana wapi, na bora habari hizo ziletwe hapa katika blogu ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...