Mwandishi wa Habari mwandamizi Bi. Celesencia Kapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakata alipotangaza nia ya kugombea udiwani kata ya NDILIMALITEMBO Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa pamoja na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Majira ambaye ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilimalitembo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) . Habari na picha na Demasho.com.
..............................................................
WAKATI watu mbalimbali wameanza kujitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa mwandishi wa habari  Mwandamizi,  Mkoani  Cresensia Kapinga ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilima litembo manispaa ya Songea  Ruvuma.

Mwandishi huyo ametangaza nia yeke ya kuwania nafasi ya udiwani  mbele ya waandishi wa habari  kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari  Mkoa wa Ruvuma  zilizopo mtaa soko kuu mkoani  humo.
Amesema kuwa  kabla ya kutangaza nia amejipima na kujiona anaweza kuongoza kata baada ya kuwa  aligombea nafasi hiyo kupitia viti masalumu mwaka 2010 ambapo kura hazikutosha.

Akijibu masawali mbalimbali ya Waandishi wa habari amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo baaada ya kuona Changamoto mbalimbali zinazowakabaili Wananchi Katika Kata hiyo iliyokonje kidogo ya Manispaa  ya songea hazijafanyiwa kazi. 

‘Ziko Changamoto nyingi zinazowakabili Wananchi  wa Kata ya Ndilimalitembo bado hazijafanyiwa kazi,baadhi zikiwa ni Ukosefu wa Zahanati,Shule kukosa Vyoo na Wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao ambazo naamini  nikipata  nafasi ya kuwa Mwakilishi wao nitazishughulikia’anasema Bi. Cresensia Kapinga.

Anasema kuwa kuwa kutokana na  na taaluma yake ya uandishi wa habari ana uwezo wa kuingia Ofisi yoyote katika Manispaa ya Songea  na kuwasemea Wananchi wa  Kata hiyo hivyo anasema ni fursa  pekee ya Wananchi hao kumpa Fursa ya kuongoza Kata hiyo.
Kwa upande wa Waandishi wa habari amesema kuwa  kwa kuwa yeye ni Mwanahabari atajitahidi kuwasema kwenye Baraza la  Madiwani  akiamini yapo mambo mengi yanashindwa kushughulikiwa ikiwemo posho zao.

Kwa upande wao Waandishi wa Habari wamepongeza hatua hiyo  na kutaka Waandishi wengine wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa Waandishi wamekuwa  wakinadi watu wengine wakati wapo baadhi yao wana uwezo wa kuongoza.

Mmmoja wa Waandishi hao Julius Konala anasema hatua hiyo ni ya kupongeza sana kwa kuwa imefunguia njia kwa Wanahabari wengine kugombea zaidi  na kuwata Wananchi  na Wanaccm kumuunga mkono  katika  azma yake ya kutaka kuwa  Diwani wa Kata ya Ndilimalitembo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...