Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amekutana na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo ili kujadili utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kulia) akizungumza na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo (hawapo pichani). Katikati ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.
Meneja Tanesco katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Mbeya, Ephraim Cheyo (aliyesimama) akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya yake, wa kwanza kushoto ni Meneja Tanesco, wilaya ya Kyela, George Fulla na wa pili kushoto Meneja Tanesco katika wilaya ya Mbinga, Kanuti Punguti. Maelezo hayo aliyatoa wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji vijijini katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi kilichofanyika jijini Mbeya.
Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (aliyesimama) katika kikao kilichofanyika jijini Mbeya ili kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika kanda hiyo.
Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi, wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili katika kanda hiyo pamoja na watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Mbeya ili kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika kanda hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...